Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Vikao mbalimbali vya kuhuishwa kumbukumbu ya Karbala na Mapinduzi Matukufu ya Imam Hussein (as) zinaendelea katika Mji wa Arusha. Kila Siku ambapo Waumini kutoka maeneo mbalimbali wanakusanyika na kuhudhuria kwa wengi katika maeneo ya Husseiniyyah na Misikitini kwa ajili ya Kusikiliza Historia halisi ya Imam Hussein (as) na Mapinduzi adhimu aliyoyafanya katika kupinga dhulma na kuhuisha Haki na Uadilifu na kurudisha Heshima ya Uislamu na Waislamu bali Wanadamu wote, mambo ambayo adui wa Uislamu Yazidi bin Muawia alilenga kutafyekelea mbali na kueneza ufisadi Mkubwa uliokithiri ardhini.
Kwa uwezo mkubwa wa Allah, Imam Hussein (as) aliweza kuandika Historia adhimu na ya kudumu kwa kusimama imara dhidi ya dhulma na utwaghuti wa Mungu Yazid bin Muawia. Na Kwa Baraka ya Harakati ya Imam Hussein (as), Muovu huyo alishindwa katika Malengo yake, na Ulimwengu ukashuhudia Mapinduzi makubwa yanayoendelea mpaka leo hii kutoa matunda yake kwa kila zama.
Your Comment